Alhamisi 20 Agosti 2026 - 08:46
Imam Shahidi alikuwa mbunifu wa kuzalisha nguvu kwa ajili ya Iran/ Taifa limesimama kulipiza damu ya kiongozi wake shahidi

Ayatullah A’rafi, huku akisisitiza kwamba kisasi, kulipiza kisasi na kudai kisasi kwa ajili ya Imam Shahidi na mashahidi wapendwa si jambo la mtu binafsi wala la kihisia, amesema: “Taifa letu limesimama kwa ajili ya kulipiza damu ya Imam Shahidi; hata ikiwa itachukua miaka sita, halitaacha kulipiza kisasi.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A’rafi, Mkuu wa Hawza nchini Iran, usiku wa jana alihudhuria hafla ya kumbukizi ya siku ya 40 ya msafara wa mazishi ya Imam Shahidi, iliyofanyika kwa ajili ya Imam Shahidi na kuandaliwa na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, katika ukumbi wa Imam Khomeini (ra) uliopo ndani ya Haram Tukufu ya Hadhrat Fatima Ma’suma (sa).

Akieleza kwamba Imam Shahidi alituzalishia nguvu katika nyanja mbalimbali, alisema: “Umma wa Kiislamu ulikuwa umedumaa katika uwanja wa sayansi na teknolojia kwa miaka 200. Kwa miaka na karne nyingi tulikuwa tumeathiriwa na utegemezi wa kisayansi na kiteknolojia kwenye nchi za Magharibi, na mambo yetu yote ya kisayansi na kiufundi yalikuwa yanategemea nchi hizo. Hata leo, sehemu kubwa ya ulimwengu wa Kiislamu bado inategemea Magharibi, lakini Imam Shahidi, katika kipindi cha miaka 40 ya uongozi na utawala wake, alifuata mkondo mmoja thabiti, nao ilikuwa ni kuzalisha nguvu ya kisayansi na kiteknolojia kwa ajili ya Iran.”

Mkuu wa Hawza nchini Iran, alisisitiza kwamba uangavu na ukubwa wa shakhsia ya Imam Khomeini (ra) na kiongozi shahidi wa Mapinduzi katika historia ya maelfu ya miaka ya Iran hauna mfano wa kulinganishwa nao.

Mjumbe wa Baraza la Walinzi la Iran, akizungumzia nguvu za kijeshi na kiulinzi za Iran katika kipindi cha uongozi wa Imam Shahidi, alisisitiza: “Imam wetu Shahidi aliijenga nguvu ya ulinzi kwa msingi wa doktrini ya kijeshi iliyoendelea sana. Uerevu wake, mtazamo wake wa kutazama mambo ya wakati ujao, pamoja na uongozi wake katika masuala ya ulinzi na kijeshi, viliifanya Iran kuwa kinara wa eneo hili na kujenga nguvu iliyoweza kusimama mbele ya madola yenye nguvu zaidi duniani. Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, mwongozo wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi na kujitolea kwa vikosi vya jeshi, msimamo huu wa kupambana na maadui utaendelea.”

Mkuu wa Hawza za nchini Iran alisisitiza kwamba; “sisi si waanzilishi wa mashambulizi, lakini katika nafasi ya kujilinda, tutakuwa washambuliaji na tutayafanya maisha ya maadui kuwa magumu.”

Ayatullah A’rafi aliendelea kwa kusisitiza kwamba; kisasi, kulipiza kisasi na kudai kisasi kwa ajili ya Imam Shahidi na mashahidi wapendwa si jambo la mtu binafsi wala la kihisia, akasema: “Kulipiza damu ya Imam wetu Shahidi si kisasi cha mtu binafsi, bali ni kisasi cha Umma wa Kiislamu na wanyonge wote duniani. Tumesimama katika kulipiza kisasi na kudai damu ya kiongozi wetu shahidi, hata kama miaka mingi itapita.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha